MWANAMITINDO anaye-tingisha kwa umbo lake matata Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ ameamua kukimbilia kwa bibi yake, Marangu mkoani Kilimanjaro kutokana na hofu ya Ugonjwa wa COVD- 19 unaosababishwa na Virusi vya Corona.
Akibonga na OVER ZE WEEKEND, Sanchi amesema aliamua kuweka pembeni mambo yote ya mjini na kwenda kijijini kwao huko hadi janga hilo lipite ndipo arudi mjini na kuendelea na mipango yake.
“Ni kweli nipo kwa bibi yangu nakula zangu ndizi, yaani huku hakuna vurugu kama za mjini, huku ni kukaa ndani ukichoka unakwenda shambani hivyo labda mwezi wa tisa ndiyo nitarudi Dar, nimeshajua na kulima vizuri tu,” alisema Sanchi ambaye alikuwa anataka kufungua duka lake la mavazi ya mazoezi na nguo za ndani liitwalo Seductive, lakini ameshindwa.