NEWS

27 Aprili 2020

MC Pilipili, Mkewe Kudaiwa Kuachana!



LICHA ya janga la Corona kuendelea kutikisa nchini na duniani kote, bado kwenye ulimwengu wa mastaa nako kulikuwa na mambo! Moja kati ya mambo yaliyotikisa wiki hii ni pamoja na ndoa ya mchekeshaji Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ na mkewe Philomena Thadey ‘Qute Mena’ kudaiwa kuvunjika.


Kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii, gumzo kubwa lilikuwa ni vijembe kuhusiana na ndoa hiyo kuvunjika, ambapo zaidi aliyekuwa anapondwa sana ni MC Pilipili.

Walimnanga kuwa tangu awali alikuwa akiwatambia sana watu mitandaoni kwamba mkewe mzuri, jambo ambalo lilikuwa likiwachefua watu kwa kumuona kama limbukeni wa mapenzi.

 

“Kiko wapi sasa, yaani watu wa namna hii wakiachagwa kama hivi ndio utawaonea huruma sababu show off zilikuwa nyingi sana, hatunywi maji bwana,” aliandika mdau mmoja mtandaoni.

Akizungumza na RISASI, MC Pilipili alisema kuwa anashangaa kuona watu kutwa kushinda kwenye mitandao na kumsema yeye na mke wake.


“Mimi sijaachana na mke wangu, bado tupo vizuri tu hata wanavyosema siku hizi siposti picha tukiwa pamoja, ni kwamba kuna muda unatakiwa ufanye mambo mengine ya kujenga familia lakini nimejua kuwa mimi ni mti wa matunda, lazima nipigwe mawe. Ndio maana huwa haipiti wiki, lazima niongelewe Mimi na Cute Mena na hata sasa hivi mtu akitaka kuja kwangu kuhakikisha, namkaribisha,” alisema MC Pilipili.