NEWS

30 Aprili 2020

Unaniume Sana 'Baada ya Kwenda Mafunzo ya JKT Mpenzi Wangu Arudi Bila Bikira'

Hello Admin, naomba nisaidie hili
mimi ni kijana wa chuo mwaka wa pili, nilitokea kumpenda binti mmoja aliyemaliza kidato cha sita 2012 ambaye alikuwa ni jirani yangu na kwel tulipendana sana ,na tulipanga mimi na yeye tuje kuoana na kutokana na mazingira aliyolelewa baba yake akiwa mchungaji aliniambia kuwa yeye ni bikira na ataitunza hadi ndoa. kwakwel niliheshimu hayo mawazo yake kwa kuwa nlkw nampenda sana had wazazi wetu walikuwa wanalitambua hilo

Ila alipomaliza kidato cha sita alitakiwa aende kwenye mafunzo ya jkt kulingana na agizo la serikali hivyo alienda huko na nlikuwa nawasiliana nae mara kwa mara ingawa sio sana.


Kitu cha ajabu amebadilika sana kitabia tangu aliporudi ,nilipomuhoji vizur alikuja kuniambia kwa ss yeye sio bikira tena..nilipomuuliza kwa nn umechukua uamuzi huo? akaniambia alikuwa amechanganyikiwa kutokana na mazoez ya jkt had akafanya mapenz bila kujitambua ila akaomba msamaha na tuishi km zamani...kwakwel nimechanganyikiwa na sijui hata nimjibu nini? naomba ushaur kwako