NEWS

28 Aprili 2020

Wasanii Tanzania Wauza SIMU zao ili Kuishi Kutokana na Ukata wa Corona


 Pepeta Asha Baraka amesema kuna baadhi ya wasanii wake wameuza simu zao ili kukidhi mahitaji yao ya kila siku wakati huu ambapo shughuli za kuwaingiza kipato wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona.

Baraka ambaye bendi yake ina wasanii zaidi ya 40 amesema hatua hiyo inatokana na ugumu wa maisha ya wasanii wakati huu ambapo kumbi nza baa zimefungwa kutokana na marufuku za mikusanyiko.


“Sasa hivi kumbi na baa zimefungwa hatupigi muziki kwa sababu ya Corona, nimewasaidia kuwalipa mshahara wanamuziki wangu kwa mwezi mmoja na mimi nimeishiwa nina wasanii zaidi ya 40, wengine wameuza simu ili wajikimu kimaisha”,