NEWS

28 Aprili 2020



Zaidi ya visa milioni tatu vya maambukizi ya virusi vya corona vimesajiliwa rasmi duniani kote, ambapo karibu asilimia 80 vimepatikana Ulaya na Marekani.

Rekodi hizo ni kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Shirika la Habari la Ufaransa AFP. Kwa namba halisi takwimu hizo zinaeleza takribani maambukizi 3,003,344 yamebainika, ikiwemo vifo 209,388, na vingi vya hivyo vimetokea Ulaya ambako kuna jumla ya maambukizi 1,393,779 na vifo 126,233.

Marekani ambako janga la virusi vya corona linasambaa kwa kasi kuna maambukizi 980,008 vikiwemo vifo 55,637.

 Idadi ya maambukizi yaliyogunduliwa inaaminika kuwakilisha sehemu tu ya idadi ya kweli ya maambukizo ya watu waliopimwa kwa sababu nchi nyingi zinashiriki katika ufanyaji wa kiasi kidogo katika jitihada za upimaji kutokana na sababu mbalimbali.