NEWS

1 Mei 2020



Moja ya Couple ambazo zinaanza kuteka mazungumzo mtandaoni kwa sasa Bongo, ni hii ya Nandy na Bill Nass mara baada ya hivi karibuni wawili hao kuingia katika hatua ya uchumba.

Kwa sasa kinachofuatia au kusubiriwa kutoka kwao ni harusi kitu ambacho kinawafanya mashabiki kuanza kunusa huku na kule ili kuweza kujua ni lini hilo litafanyika.

Akiwa Insta Live, Nandy amesema kuwa harusi yake hiyo itarushwa Live kwenye TV ingawa hajaweka wazi ni lini hasa itafanyika. Pia Nandy alijibu swali la iwapo kwa sasa anaishi pamoja na BillNass, “Kitanzania sio sawa kuishi wote hadi mfunge ndoa”.

Utakumbuka pia msanii Alikiba wakati ameona harusi yake ilirushwa Live kupitia AzamTV kutoka kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam, baada ya sherehe fupi ya kufunga ndoa iliyofanyika Mombasa nchini Kenya.