Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini anayemaliza muda wake Zitto Kabwe, ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo kwa mara nyingine tena.
Kupitia Ukurasa wake wa kijamii wa ‘twitter’ Zitto ameandika kuwa huu ndio wakati muhimu kwa historia ya demokrasia na yuko tayari kugombea ubunge Kigoma mjini.
“Huu ni wakati muhimu zaidi katika historia ya demokrasia ya Vyama vingi nchini. Ni wakati wa kuhami demokrasia yetu. Ni wakati wa kuhakikisha tunaunda Serikali ili kurejesha furaha kwa Watanzania. Nimeamua kuwa Nitagombea Ubunge Kigoma Mjini”, ameandika Zitto.
Watia nia Ubunge Kigoma mjini mpaka sasa kupitia ACT-Wazalendo ni Zitto Kabwe, Abdul Nondo, Hussein Kaliango na Idd Adam