NEWS

20 Julai 2020

Huwezi Amini Rais Magufuli Ataka Kura Zihesabiwe Hadharani



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt John Magufuli, amesema katika nafasi ya Ubunge jumla ya waliojitokeza kutia nia ya kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya vhama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba ni 10, 367.


Rais amesema hayo leo Julai 20, 2020 wakati akizungumza na viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni mara baada ya kuwaapisha Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, ambapo ameagiza kura za maoni zihesabiwe hadharani.

"Ni kweli mmepata nafasi hizi kwa sababu ya fursa nina imani mlioteuliwa mtakwenda kutekeleza wajibu wenu, mpaka leo waliochukua fomu za Ubunge na uwakilishi kupitia CCM ni 10,367 na waliorudisha fomu ni 10321, kwahiyo ambao hawakuzirudisha ni 46", amesema Rais Magufuli.

Julai 14 hadi 17 chama hicho kilifungua dirisha la uchukuaji fomu kwa watia nia wa nafasi za Ubunge na Udiwani, ambapo imeshuhudiwa maelfu ya watia nia tofauti na chaguzi zilizopita na huenda uchaguzi wa mwaka 2020, ukawa umeweka rekodi ya pekee.