GAZETI la mtandaoni la KINEDA limeripoti habari yenye msisimko wa kipekee, ambapo mwanamme mmoja aitwaye Jian Feng, amemshitaki mkewe kwa kumzaliwa watoto wenye sura mbaya.
Feng anasema alimuoa mkewe kwa furaha na upendo, lakini furaha hiyo imetoweka na kuwasababishia mfarakano wa kindoa baada ya mkewe huyo kumzalia watoto wenye sura mbaya kiasi hata cha kuwaogopa.
Kwa kujitazama utanashati wake, pamoja na urembo wa mkewe, Feng hakuamini kama watoto wale wangekuwa ni wa kwake, hivyo alimshutumu mkewe kwa kukosa uaminifu katika ndoa. Lakini, hata hivyo, vipimo vya DNA vilithibitisha kuwa watoto wale ni wa kwake.
Kwa bahati, baadaye mke wa Feng, alikuja kukikiri wazi na kuthibitisha kwamba, huko nyuma kabla hawajafunga ndoa, alipata kutumia kiasi cha dola $100,000 (€77,000) kufanyiwa upasuaji nchini Korea Kusini wa kujibadili mwonekano wake (cosmetic surgery).
Kufuatia kukiri huko, Feng alimshitaki mkewe kwa kosa la kugushi mwonekano, na kutosema kweli juu ya upasuaji aliofanya kiasi cha kusababisha aonekane mrembo kinyume na uhalisia. Jaji alikubaliana na malalamiko ya Feng, na kumtaka mke alipe fidia ya dola $120,000 (€102900).