MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema kwamba iwapo atateuliwa kuwa Rais wa Zanzibar atahakikisha anapiga vita na kupambana kwa nguvu zake zote suala zima la udhalilishaji wa wanawake na watoto visiwani humo.
Amesema kwamba vitendo vya udhalilishajui wa Wanawake na watoto visiwani Zanzibar vimekithiri kwa kiasi kikubwa hivyo endapo wazanzibar watamchagua kuwa rais wa Zanzibar atahakikisha kwamba anapambana na vitendo hivyo kwa nguvu zote.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi CCM ambapo ufunguzi huo umefanyika katika viwanja vya Demokrasia, Kibanda maiti Mkoa wa Mjini Unguja na kuhudhuriwa na maelfu ya wanachama wa chama hicho visiwani Zanzibar.
Dk Mwinyi amesema kuwa kwa muda mrefu visiwani vya Zanzibar vimekabiliwa na kadhia ya udhalilishaji wa wananwake na watoto pamoja na kuwepo kwa vitendo vya dhulma, uonevu na kushairi kwa dawa za kulevya hivyo ewapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar
Pia amesema endapo atachaguliwa atahakikisha kuwa anauwa mkali na upambana na watendaji wa serikali ambao hawawajibiki kazini sambamba na watendaji wanaokula rushwa.
Katika maelezo yake Dk Mwinyi amesema kwamba atahakikisha anakuza utalii wa Zanzibar ambao utafungua fursa za ajira kwa vijana.
“Utahakikisha tunazalisha ajira laki tatu kwa mwaka ambapo zitakwenda kuwasaidia vijana wenu ndani ya visiwa hivi”amesema DK Mwinyi.
Hata hivyo amesema kwamba atahakikisha anakuza uchumi wa Zanzibar ambao utakwenda sambamba na ujenzi wa viwanja vya ndege na kuboresha miondombinu ya barabara.
“Ndugu zangu wananchi katika huduma za kijamii ntahakikisha kwamba tunaboresha huduma zote muhimu za kijamii kama vile elimu bure, maji safi na salama pamoja na hudua za afya ambazo zitatolewa bure,”ameeleza Dk Mwinyi.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Dk Abdullah Juma Saddala (Mabodi) akiichambua ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025 alisema, ni ilani ambayo inatekelezeka.
Alisema, Ilani hiyo imesema itaendeleza jitiihada za kuunganisha wazanzibar wote na kuwa wamoja lakini pili kuhakikisha maendeleo ya uchumi yanazngatia usawa na yananufaiha maeneo yote ya Zanzibar kwa maana ya Unguja na Pemba.
Lakini pia alisema, ilani ya chama cha Mapinduzi pia itaendelea kuwanafaisha wananchi wa nafasi zote pamoja na kuimarisha upatikanaji wa ajira kwa vijana.
Lakini pia amesema, jambo jengine ambalo lipo katika ilani hiyo ni kupitia upya mfumo wa elimu wa ufundi wa amali ili vijana wengi waweze kupata ajira.
Aidha amesema, jambo jengine ni kuibua na kueneleza sekta mpya ya uchumi ambao ni uchumi wenye ubunifu, uchumi unaotekelezeka na uchumi wa kidigitali.
Nae MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein akimuombea kura mgombea urasi wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Mgombea urasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli pamoja na wabunge, wawakilishi na madiwani wote wa CCM.
Amesema, Dk Hussein Ali Mwinyi ana kila sifa za kuiongoza Zanzibar kwa kuwa Rais wa Zanzibar kwani ana uwezo mkubwa sana na sio mwanagenzi katika siasa kwani ameshawahi kuongoza katika majimbo mawili akiwa mbunge likiwemo Jimbo la Mkuranga na la kwa hani.
Amesema, alisema anamfahamu vizuri Dk Mwinyi na ana uwezo mkubwa wa kuiongoza Zanzibar na ndio maana chama kimemteua kuweza kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia chhama hicho.
Amefahamisha kuwa, Dk Mwinyi ana uwezo mkubwa sana kwani taaluma yake ni Daktari bingwa wa binaadamu na ni mtu aliyesoma akabobea na ni muhadhiri wa chuo kikuu.
Katika Ufunguzi huo wa kampeni wasanii mbali mbali wa filamu, Bongo fleva pamoja na vikundi mbalimbali vyataarabu kutoka Zanzibar na Bara vimewaburudisha wanachama wa chama hicho.