NEWS

14 Septemba 2020

Hussein Mwinyi: Mkiniteua Kuwa Rais wa Zanzibar nitaondoa Dhulma na Upendeleo Wakati wa Utoaji wa Kazi Serikali



MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema kwamba iwapo atateuliwa kuwa Rais wa Zanzibar atahakikisha anaondoa dhulma na upendeleo wakati wa utoaji wa kazi Serikali.

Amesema anatambua kuwa upatikanaji wa ajira  za Serikali kumekuwa na dhulma na upendeleo kwa baadhi ya watu wenye uwezo, hivyo endapo atateuliwa na wananchi wa Zanzibar kuwa Rais atahakikisha anaondoa suala hilo.

Hayo ameyaeleza leo wakati wa Ziara maalumu ya kuwatembelea wananchi mbalimbali katika mkoa wa kusini ikiwa ni muendelezo wa kampeni za chama cha Mapinduzi ccm visiwani humo.

Dk Mwinyi amesema lengo la kugombea nafasi ya Uras wa Zanzibar ni kuhakiksha anatatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo na suala zima la dhulma na upendeleao wakati upatikanaji wa ajira za serikali.

Amefahaamisha kwamba suala la dhulma na upendelo wa kazi serikali ni suala ambalo linatatulika na atahakikisha wananchi kila mmoja anapata haki na fursa sawa wakati wa upatikanaji wa ajira Serikalini.

Aidha Dk Mwinyi amesema kwamba iwapo atakuwa rais ataweka utaratibu maalumu wa kuwafata wananchi katika maeneo waliyopo kwa lengo la kusikiliza changamoto walizonazo na kuwatatulia.

Hata hivyo amesema atafanyia kazi ya ziada sul zima la udhalilishaji ambapo kila sehemu anayo kwenda anakumbana nalo.

Amesema atahakikisha atenga nguvu ya pamoja baina ya Serikali na wananchi katika kuliondoa suala zima la udhalilishaji wa Wanawake na watoto visiwani humo.

Nao wakazi wa Kizimkazi Dambani  walisema kuwa changamoto kubwa wanayokabiliwa ni upatikanaji wa ajira kwa vjana wao ambapo wanafanya maombi ya kaz lakini dhumla na upendeleo huwa inwasumbua.

Pia wamesema kwamba upatikanaji wa maji na salama katika eneo lao bado ni changamoto ambayo inawakabili kwa muda mrefu.