MGOMBEA wa Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amewekewa pingamizi na kushindwa kuteuliwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi kuwa mgombea wa urais hadi pale pingamizi litakapo sikilizwa na kutolewa maamuzi.
Mkurugenzi huyo amesema kwamba muda wa pingamizi uliwekwa kwa masaa 24 umekamilika na mgombea wa chama cha ACT wazalendo Maalim Seif Sharif Hamadi kuwekewa pingamizi na chama cha DP na Democrasia Makini kumuwekea pingamizi la kushindwa kukamilisha baadhi matakwa katika fomu hizo.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za Tume Mkurigenzi wa ZEC Thabit Idarous Faina huko Maruhubi Mjini Magharib Unguja.
Aidha Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC imepitisha jumla ya wagombea 16 kati ya 17 kuwa wagombea na nafasi ya urais na kuanza kampeni siku ya tarehe 11 mwezi huu.