NEWS

28 Septemba 2020

Mahakama yazuwia kwa muda marufuku ya TikTok nchini Marekani



Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu nchini Marekani ameahirisha kutekelezwa kwa amri ya Rais Donald Trump kuipiga marufuku programu ya TikTok nchini Marekani, iliyokuwa ianze kutekelezwa usiku wa manane kuamkia leo. 

Hata hivyo, marufuku hiyo inaweza kutekelezwa kuanzia mwezi Novemba, wiki moja baada ya uchaguzi mkuu wa Marekani. Jaji Carl Nichols hakukubaliana na kuahirishwa kwa marufuku hiyo mwezi Novemba. 


Uamuzi huu wa jana unafuatia hati ya dharura ambapo mawakili wa TikTok walihoji kwamba marufuku hiyo ingelivunja haki za kikatiba za kampuni ya wateja wao na kusababisha madhara yasiyolipika kwenye biashara. 


Mapema mwaka huu, Rais Trump alitangaza kwamba programu hiyo ya video kupitia simu za mkononi ni hatari kwa usalama wa taifa na akaamuru ama inunuliwe na kampuni za Kimarekani au ipigwe marufuku moja kwa moja.