NEWS

28 Septemba 2020

Nandy Afunguka Ukweli Wote Kunasa Mimba ya Billnas



MREMBO anayefanya poa kwenye Bongo Fleva, Faustine Charles ‘Nandy’, ameweka wazi kuwa hana ujauzito ila mwili wake umeongezeka kwa sababu ya mabadiliko ya binadamu.

Nandy amesema mashabiki wameanza kumnyooshea vidole kuwa tayari amenasa ujauzito wa mchumba wake, Billnas, jambo ambao sio kweli.


“Watu wanasema mimi ni mjamzito kwa sababu nimenenepa, ukiangalia familia yetu wote wana maumbo makubwa halafu ni wanene labda na mimi ndiyo nimefikia hatua ya kuwa hivyo, sina mimba,” alisema Nandy.