Wabunge katika Jimbo la Kaduna nchini Nigeria wamepitisha adhabu ya kuwahasi wale wataokutwa na hatia ya kuwabaka watoto walio chini ya umri wa miaka minne.
Gavana wa jimbo Nasir Ahmad el-Rufai anatakiwa kutia saini mudwada huo ili kuwa sheria katika jimbo hilo la Kaskazini Magharibi.
Awali aliunga kono adhabu hiyo ili kudhibiti vitendo vya ubakaji kujirudia, Sheria nchini Nigeria inaelekeaza adhau ya kifungo cha miaka 14 na kifungo cha maisha, lakini wabunge wanaweza kuweka adhabu ya tofauti.
Unyanyapaa huwafaya waathirika kushindwa kuripoti matukio ya ubakaji nchini Nigeria na idadi ya watu waliofikishwa kwenye vyombo vya sheria ni ndogo