Msanii wa filamu Niva Supa Marioo ameeleza kuwa kwenye maisha yake hajawahi kwenda jela ila aliwahi kuingia mahabusu kwa sababu ya kumpiga mpenzi wake wa zamani baada ya kumfumania.
Niva Marioo amesema alipelekwa mahabusu mara mbili mara ya kwanza ni baada ya kumfumania mpenzi wake, mara ya pili alikamatwa baada ya kwenda kufanya show na marehemu Udeude.
"Kwenye maisha yangu sijawahi kwenda jela, ila polisi na mahabusu niliwahi kuingia mara mbili, kosa la mara ya kwanza ilikuwa kumpiga Ex wangu ambaye nilimfumania, kama unavyojua unapomfumania mtu unakua kama kichaa, tena nilimfuma akiwa anapigwa kiss na mwanaume mwingine kwenye gari, nilikuwa nimemfuata tuka-enjoy na kula bata ila nikajikuta nimelala kituoni"
Niva Marioo amesema baada ya tukio hilo kutokea alikaa chini na kujutia kwa sababu ndiyo ilimfanya aweze kwenda polisi kwa mara ya kwanza.