NEWS

5 Septemba 2020

Rungwe Amesema Atatumia Ubwabwa Kama CCM Wanavyotumia Wasanii.."Nitaenda Mahakamani"



Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Ilala, Christopher Myava amemuonya Hashim Rungwe ambaye ni mgombea Urais kupitia CHAUMMA kuwa kugawa chakula ‘ubwabwa’ wakati wa kampeni ni rushwa na ni kosa kisheria

Myava alisema Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 inapiga marufuku kwa mgombea kutoa vitu kama chakula kushawishi wapigakura ili wamchague. Rungwe amekuwa akiwaalika wafuasi wajae kwenye kampeni zake ikiwemo uzinduzi utakaofanyika Manzese, Dar es Salaam leo Septemba 5 kwa kuahidi ubwabwa utakuwepo

Myava amesema kipindi hiki kinachotakiwa ni kunadi sera ili kuomba ridhaa ya wananchi kumchagua na si kushawishi kwa kutoa rushwa.

Rungwe amesema atatumia ubwabwa kama CCM wanavyotumia wasanii. Amesema kufanya hivyo si rushwa. Na amewataka wajiandae kupelekana mahakamani

Maoni ya wadau wengi wa JamiiForums yanahoji “Je, kutumia wasanii kufanya maonesho bure katika kampeni sio rushwa?”