NEWS

13 Novemba 2020

Magufuli "Tunahitaji Mabilionea Wengi wa Kitanzania"

 


"Tunataka mtu yeyote anayetaka kuwekeza asisumbuliwe....Watanzania ni matajiri lakini baadhi yao wanaogopa kuwekeza hapa nchini wakiogopa kusumbuliwa kwa maswali yasiyo na msingi. Tunahitaji mabilionea wengi wa Kitanzania." Ni sehemu ya hotuba ya Rais Dkt Magufuli akizindua #BungeLa12.


Rais amesisitiza kwamba katika kipindi miaka 5 ijayo Serikali yake itaongeza jitihada za kukuza uchumi, kupambana na umaskini na kuongeza ajira. Amesema Serikali itazalisha ajira 8,000,000.