NEWS

13 Novemba 2020

“Nataka Mwekezaji akitaka kuwekeza Tanzania apewe kibali ndani ya siku 14- JPM



 “Nchi yetu inashika nafasi ya pili kwa mifugo mingi Afrika, tutainua Sekta ya Mifugo ikiwemo kukamilisha ujenzi wa Machinjio 7 Nchini,tunakaribisha Wawekezaji kuwekeza kwenye bidhaa za mifugo ikiwemo viwanda vya ngozi, nguo,mikanda nk, tutanunua 8 za uvuvi'' Rais MAGUFULI Akiwa Bungeni

“Nataka Mwekezaji akitaka kuwekeza Tanzania apewe kibali ndani ya siku 14 na katika hili nimeamua suala la uwekezaji ikiwemo kituo cha uwekezaji (TIC) kulihamishia Ofisi ya Rais kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, ili wanaokwamisha wapambane na Mimi moja kwa moja” Rais MAGUFULI Akiwa Bungeni