NEWS

13 Novemba 2020

Rais Magufuli "Lengo la Demokrasia ni Kuleta Maendeleo na Sio Fujo"

 


Akiwa Bungeni Dodoma amesema lengo la Demokrasia ni kuleta Maendeleo na sio fujo kwasababu hakuna #Demokrasia isiyo na mipaka wala hakuna Uhuru na Haki isiyo na wajibu, aidha vyote vinakwenda sambamba


Kwa miaka mitano ijayo, amesema Serikali inalenga kukuza na kuimarisha Demokrasia na kulinda uhuru na haki za Wananchi pamoja na Vyombo vya Habari


Amewaambia Wabunge ushirikiano anaoutaka kutoka kwao hauna maana wakubali na kupitisha kila kitu. Amewataka kukosoa pale panapohitaji kukosolewa, lakini wakosoe kwa lengo la kuboresha na kujenga, si kukosoa tu kwa lengo la kukosoa.