NEWS

23 Machi 2021

Rais Mwinyi Awataka Watanzania Kuendelea Kumtegemea Mungu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwa wamoja, katika kipindi hiki cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli.

Amesema katika uhai wake Dkt Magufuli alisisitiza umoja, mshikamano, amani na upendo miongoni mwa Watanzania, hivyo ni vema Watanzania wakaendelea kuwa Wamoja ili kumuenzi Kiongozi huyo.


Rais Dkt Mwinyi amesema kifo cha Dkt Magufuli kimeleta majonzi makubwa pande zote mbili za Muungano, lakini cha kufanya hivi sasa ni kumuomba mwenyezi Mungu na kumuombea Marehemu.

Ameahidi kushirikina na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ili kutimiza ndoto za Dkt Magufuli za kuwaletea maendeleo Watanzania wote.

Amesema anatambua uwezo mkubwa wa Rais Samia katika masuala ya uongozi, hivyo hana shaka na anaamini mambo yote yatakuwa sawa.