NEWS

30 Aprili 2021

Maandalizi Ya Mei Mosi Kitaifa Jijini Mwanza Yakamilika


Maandalizi kwa ajili ya sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zinazotarajiwa kufanyika kitaifa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza hapo kesho yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Eenye ulemavu, Jenista Mhagama amesema  maandalizi yote muhimu kwa ajili ya sherehe hizo yamekamilika.

Kwa mujibu wa Waziri Mhagama, Mgeni rasmi katika sherehe hizo ni Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na kutoa tuzo kwa Wafanyakazi waliofanya vizuri katika sekta mbalimbali.

Aidha, amewahimiza Wananchi wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki katika sherehe hizo za kitaifa za Mei Mosi.

Kauli mbiu ya sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani kwa mwaka huu kitaifa ni “Maslahi Bora, Mishahara Juu, Kazi iendelee”.