NEWS

28 Aprili 2021

Wabunge wataka wazee wa mabaraza kuongezewa posho


Wabunge  wameishauri Serikali kurejea upya viwango vya posho za wazee wa mabaraza ya Sh5,000 kwa kesi wakidai ni fedha kidogo.

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti, Sillo  Baran ameyasema hayo leo Jumatano Aprili 28, 2021 wakati akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya mfuko wa mahakama kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Amesema kamati inaendelea kuishauri Serikali kuhusu kurejewa upya kwa viwango vya posho za wazee wa mabaraza ambao wanalipwa Sh5,000 tu kwa kesi kiasi ambacho ni kidogo  ikizingatiwa muda unaochukua kesi kuamuliwa.

“Hatua hii itasaidia kuziba mianya ya rushwa lakini pia itaongeza motisha, tija na ufanisi katika kazi za mabaraza husika,” amesema.