NEWS

1 Mei 2021

Rais Samia aagiza wenye elimu ya darasa la saba walioondolewa kazini kulipwa mafao yao


Serikali imeagiza wafanyakazi wote wenye elimu ya darasa la saba walioondolewa kazini lakini hawakughushi vyeti walipwe mafao na stahiki zao zote.

Agizo hilo limetolewa leo Jumamosi Meimosi, 2021 mkoani Mwanza na Rais Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi iliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza.

"Wapo waliosita kutekeleza maelekezo ya malipo haya kwa kisingizio cha kutotolewa mwongozo, mwongozo ndio huo sasa nimetoa," amesema Rais Samia.