NEWS

16 Juni 2021

Mzee Matata wa Mizengwe afariki Dunia


Mchekeshaji kutoka kundi la Mizengwe Jumanne Alela (Mzee Matata) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taaarifa hizo zimethibitishwa na Mchekeshaji mwenzie wa Mizengwe Mkwere ambaye awali aliweka video akiwa analia kwenye ukurasa wake wa Instagram ambayo ilifuatiwa na post ya taarifa za kifo cha Mzee Matata.

June 13,2021 Katibu wa Chama Cha Waigizaji (TDFAA)- Wilaya ya Kinondoni alitoa taarifa ya kuugua kwa Mzee Matata ambayo ilielezea kuwa hali yake ni mbaya na amelazwa Muhimbili.