NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI inatarajia kutoa mbegu bora za alizeti kwa wakulima kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kukabiliana na upungufu wa mafuta ya kula hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa jana Wilayani Igunga na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya masoko ya pamba na kuhamasisha wakulima wa zao hilo kulima kwa wingi alizeti, choroko, dengu na pamba yenye.
Alisema nchini inakabiliwa na upungufu mafuta ya kula zaidi ya lita laki nne ili kuziba pengo kunahitaji alizeti milioini 1.3 kwa mwaka kwa ajili ya kuviwezesha viwanda kulizalisha mafuta mwaka mzima.
Bashe alisema ili kiwango hilo kiweze kufikiwa kunahitajika tani 3,900 za mbegu bora za alizeti na kuongeza kuwa Serikali imekusudia kugawa mbegu kwa ruzuku.
Alisema Serikali imeshatenga katika bejeti ya Wizara kilimo fedha kwa ajili ununuzi wa mbegu bora ambazo zitatolewa kwa wakulima ambapo watalipa nusu ya gharama baada ya kuvuna na kuuza alizeti yao.
“Kupitia fedha tulizotenga katika bajeti yetu tutaagiza mbegu ambazo tunaupungufu ndani nchi na Wakala wa Mbegu Bora za Kilimo nchini – ASA ndio atakayeagiza na Serikali itazigawa kwa wakulima kwa nusu ya bei ya aina ya mbegu”alisema
Bashe alisema wakulima wa Igunga watakiwa kulima pamba alizeti choroko na dengu kwa wingi ili kuwawezesha kuwa kipato cha kutosha kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo alisema kuanzia sasa zao la dengu na choroko hazitumia mfumo wa mauzo ya stakabadhi ghalani na badala yake mkulima atauza kule alipo.
Alisema katika kuhakikisha Mkulima aibiwi mazao yake uongozi wa Halmashauri ambazo wakulima wake wanalima mazao hayo waka na sehemu maalumu za kuuzia na kuweo na vipimo rasmi.
Bashe alisema ni marufuku kwa wanunuzi kutumia ndoo ambazo ndio zimekuwa zitumia kuwanyonya wakulima wa dengu na choroko.
mwisho