NEWS

20 Juni 2021

TECNO Yazawadia Wateja Wa TECNO Camon 17 Zawadi Mbalimbali


Kampuni ya simu za mkononi TECNO ya zawadia washindi wa promosheni ya twende zetu camping kistaa ticket za kutembelea Mbuga za Wanyama Tanzania, fridge, drones na Kinga’amuzi cha DSTV. Promosheni hii ilianza rasmi baada ya uzinduzi wa TECNO Camon 17 simu iliyobeba sifa kuu ya camera ikiwa na MP48 na MP64 nyuma. 


Kampuni ya Simu imetoa zawadi kwa wateja wa TECNO Camon 17 na washiriki wa challenge ya TECNO Camon 17 ambayo ilikuwa ikiendelea @tecnomobiletanzania kupitia drow kuu la bahati lililochezeshwa na Msanii maarufu Elizabeth Michael katika duka la simu TECNO Smart Hub Kariakoo.
 

TECNO iliwazawadia zaidi ya washindi 30 ticket ya kutembelea Mbuga za Wanyama Tanzania, fridge ving’amuzi vya DSTV na drones.


TECNO inawataka wadau wa simu za mkononi kutembelea maduka ya TECNO mara kwa mara pindi wanapokuwa na nafasi au tembelea  www.tecno-mobile.com