Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (MB) ametembelea Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyopo Jijii Arusha.
Mhe. Balozi Mulamula amefungua Mkutano wa Mashauriano wa Mabalozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa Taasisi za Jumuiya hiyo yenye makao yake Makuu jijini Arusha.
Mhe. Mulamula kwanza amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt.Peter Mathuki na baadaye amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki Mhe. Jaji Nestory Kayobera katika Makao Makuu ya jumuiya hiyo.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Mulamula pia amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe.Martin Ngoga. Mikutano kati ya Mhe. Waziri na Mhe. Ngoga umefanyika katika Makao Makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.