NEWS

13 Januari 2014

Batuli Afunguka : Sipo kwenye mahusiano, na I’m still searching

Msanii wa filamu nchini, Yobnesh Yusuph aka Batuli amesema hayupo kwenye mahusiano ya mapenzi, akidai bado anatafuta.


Akizungumza na mtandao wa Swahiliworldplanet, Batuli amesema ingawa yupo ‘single’ mwaka huu anatarajia kwenda kusoma ili kuongeza maarifa.

“Sipo kwenye mahusiano bado nipo single and I’m still searching,” amesema mrembo huyo. “Malengo yangu mwaka huu panapo uzima ni kukamilisha suala la shule. Fans wangu wajiandae kumuona Batuli mpya. Kusoma nitasoma hapa hapa ila kwa baadaye nitavuka nje and kwasasa najikita zaidi kwenye general knowledge wakati huo huo naendelea kufanya movies.”

Pamoja na filamu zingine, Batuli ameigiza kwenye filamu kama Fake Smile na Waves Of Sorrow.

Source: Swahiliworldplanet