NEWS

13 Januari 2014

Ommy Dimpoz Kufanya Show kali London Feb 15, katika Valentien day .

Mashabiki wa Ommy Dimpoz jijini London, Uingereza watashuhudia show ya aina yake ya hitmaker wa Tupogo, Ommy Dimpoz kwenye show yake ya Valentine’s Day itakayofanyika February 15.


Ikipewa jina ‘Valentine’s Love Zone, show hiyo itashereheshwa na mtangazaji wa show ya Mkasi, Salama Jabir. Pamoja na ngoma zake za awali, Nai Nai, Baadaye, Me and You na Tupogo, Ommy Dimpoz ameiambia Bongo5 kuwa watakaohudhuria show hiyo watasikia ladha mpya.

“Nitakaperform nyimbo mpya mbili ambazo hazijasikika kokote. Itakuwa show ya KiVIP zaidi,”amesema Ommy.

Amesema ameamua kumchukua Salama Jabir kama host wa show hiyo kwakuwa ana mashabiki wengi na anakulika nchini humo