NEWS

19 Januari 2014

Flaviana Matata Foundation Yazindua Rasmi Back To School Project

Siku ya tarehe 17/1/2014 ndiyo siku ambayo FLAVIANA MATATA FOUNDATION walizindua rasmi project yao mpya ijulikanayo kwa jina la BACK TO SCHOOL Project. Project hii mpya inamalengo ya kusaidia karibu wanafunzi 2500 mwaka huu ambao hawana uwezo wakupata vifaa vya masomo, foundation hiyo itatoa masaa kwa njia ya kuwasambazia vifaa vya shule/#FMFStationerykit. kwa ajili ya mafunzo shuleni.


Kupitia project hiyo mpya ya BACK TO SCHOOL, kila mwanafunzi atafanikiwa kupata madaftari kumi na mbili(12) kwa ajili ya kuandikia, peni tatu(3), penseli mbili(2), ufutio, kompasi la mahesabu(mathematical set ) na begi la mgongoni kwa ajili ya kubebea vifaa hivyo vy shule watakavyopewa wanafunzi hao.