NEWS

22 Machi 2017

Nape - Nampeleka Makonda kwa Rais Magufuli...!!!


Waziri wa habari,sanaa,utamaduni na michezo Mhe Nape Nnauye amesema kuwa ataiwasilisha ripoti ya uchunguzi wa tukio la kuvamiwa kwa kituo cha clouds media kwa Rais Magufuli.

Nape amesema hayo leo hii wakati alipokuwa akipokea ripoti hiyo ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na watu mbalimbali pamoja na wadau wa habari ambao walitaka kujua nini kitafuata mara baada ya tume aliyoiunda juzi kukamiliha kazi yake hapo jana.