Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam,Paul Makonda amegundulika kuwa Aliwalazimisha na kuwatishia kuwafunga kifungo cha miezi sita jela watangazaji wa kipindi cha Shilawadu cha Clouds Tv.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam,wakati ambapo kamati iliyoundwa kuchunguza sakata la mkuu huyo wa mkuo kuvamia kituo cha clouds media ilipokuwa inakabidhi ripoti yake kwa Waziri a habari ,sanaa,utamaduni na michezo Mhe Nape Nnauye.
Katika ripoti hiyo,kamati imebainisha kuwa Makonda Aliwasili clouds na moja kwa moja akaingia studio ambapo kipindi kilikuwa kinaendelea,ambapo aliwalazimisha wafanyakazi wa clouds paoja na watangazaji wa kipindi cha shilawadu kukirusha kipindi alichkuwa akikitaka.
Baada ya kujibiwa kuwa haiwezekani kufanya jambo hilo,makonda aliwatishia wafanyakazi wa clouds kuwa atawataja kwenye orodha ya wahusika wa madawa ya kulevya.