Katika hali isiyokuwa yakawaida,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda Alikimbia kuhojiwa na kamati ya kuchunguza sakata la kuvamia kituo cha clouds media iliyoundwa na Waziri wa Habari Sanaa,Utamaduni na Michezo Mhe Nape Nnauye.
Mwenyekiti wa kamati hiyo hii leo amebainisha kuwa walipokwenda ofisini kwa Makonda Aliwasubirisha nnje kwa zaidi ya saa tatu ambapo alikuja msaidizi wake akawaaambia Makonda Ametoka kidogo hivyo waendelee kumkoja,
Akazidi kubainisha kuwa wakati wanamngoja Makonda Alitumia mlango wa nyuma na kuwakimbia bila ya wao kujua hali iliyowafanya wakae ofisini hapo hadi saa tisa mchana ambapo waliamua kuondoka.