NEWS

22 Machi 2017

Ridhiwani: Tumeishi na RC wa Dar Vizuri Ila Kutajwa Kwenye Madawa, Kama Familia Tunamwachia Mungu...!!!


Baada ya kuitwa kuhojiwa kuhusu tuhuma za kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema taarifa hizo zilitingisha familia yake, lakini baba yake Jakaya Kikwete alimtia moyo.

Tofauti na watuhumiwa wengine waliohojiwa kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya, Ridhiwani hakutangazwa hadharani badala yake aliitwa kimyakimya na kuhojiwa na baadaye kuruhusiwa aendelee na shughuli zake baada ya kuonekana hana hatia.

Katika mahojiano maalumu na Mwananchi Digital yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Ridhiwani amesema JK hakushtushwa na badala yake alimpa nguvu ya kwenda kueleza ukweli .

“Pengine aliamua kuficha hofu yake ili kunitia nguvu,” amesema Ridhiwani.