NEWS

22 Machi 2017

Rayvanny Akataa Penzi la Jimama la Kenya...!!!!


STAA wa Bongo Fleva ambaye ni memba wa Lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’ inayomilikiwa na msanii mkubwa nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Raymond ‘Rayvanny’ amekataa ofa ya penzi iliyotolewa na mwanamke mmoja kutoka Kenya, anayetambulika kwa jina la Mishi Dorah.

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, wiki iliyopita, mwanamke huyo wa makamo, anayeonekana kuwa mkubwa kiumri kwa staa huyo wa Wimbo wa Bado, alisikika akisema kuwa anampenda mwimbaji huyo aliyeshirikishwa na Diamond katika Kibao cha Salome na kwamba atafanya kila awezalo ili aje nchini, kukutana na hatimaye kumpa penzi.

“Ninampenda Rayvanny, nitamtafuta kwa udi na uvumba nimtunuku penzi ili roho yangu itulie, nampenda sana kwa kweli,” alisema shabiki huyo.

Baada ya kutoka kwa taarifa hizo, wadau mbalimbali kwenye mitandao hiyo, walionekana wakimponda mwanamke huyo, wakimtaka kuachana na mambo hayo kwani hana sifa za kuwa na Rayvanny.

Baada ya kupata habari hizo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Rayvanny ambaye alikiri kuona habari za mwanamke huyo na kudai amekuwa akimchafua sehemu mbalimbali.

“Yaani sitaki kumuongelea kabisa huyo mwanamke, maana naona amepanga kunichafua kwani nilienda Kenya wakati f’lani nikakuta habari zake, huku nyumbani Bongo ndiyo hivi tena, sina cha kuongea maana mtu akiamua kukuchafua huwezi kuongea kitu,” alisema mwimbaji huyo.