NEWS

22 Machi 2017

Noma Sana..Mchungaji Msigwa Atoa ya Moyoni Kuhusu Rais Magufuli Kuendelea Kumnyamazia Makonda..!!!


Abraham Lincoln...mmoja wa marais wa zamani wa USA alipata kusema serikali bora ni ile ya watu, inayotokana na watu, kwaajili ya watu". Katiba ya Jamhuri ya Muungano imesisitiza kuwa wananchi ndiyo msingi wa madaraka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yote kutoka kwa wananchi. Katika ulimwengu wa kidemokrasia, kushirikisha na kuheshimu maoni ya wananchi ndiyo njia ya kwanza na ya msingi kabisa kwa serikali kutimiza mamlaka ya mwisho waliyonayo wananchi. 

Sasa huyu anayepuuza maoni, malalamiko na ushahidi wa wazi wa wananchi dhidi ya Bashite, amepoteza sifa zote za uongozi zinazokubalika duniani. 

Baba wa Taifa, Nyerere, alipata kusema "madaraka hulevya, na madaraka zaidi hulevya zaidi"

Huyu anayesema hapangiwi, haonyweshi njia ya kupita, eti aliamua mwenyewe kuwa Rais baada ya kujiona anafaa; huyu anayedhani kujiamini ni kutosikiliza wananchi na kumlinda yule ampendaye yeye tu; sio Kiongozi tena. Ni Mlevi wa Madaraka. Hii ni fursa nyingine kwa Watanzania kutafakari na kuchukua hatua sahihi dhidi ya hatari inayotukabili ya kuendelea kuongozwa na Mlevi

Pale uvunjaji wa sheria na ukosefu wa haki inapokuwa , jambo la kawaida katika jamii yetu .hasa inapofanywa na viongozi wetu ,kuipinga hali na tabia hiyo inapaswa kuwa wajibu wetu sote!
Peter Msigwa The MP