MFUNGAJI Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Emmanuel Okwi, bado anateswa na hat trick aliyoifunga Oktoba 28, 2018 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Okwi ambaye alifunga hat trick hiyo wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0, tangu wakati huo mpaka sasa bado hajafunga bao lolote kwenye ligi hiyo akiwa nayo mabao saba.
Mshambuliaji huyo raia wa Uganda, kwa sasa amepitwa mabao manne na kinara wa ufungaji msimu huu, Heritier Makambo wa Yanga ambaye ana mabao 11.
Wakati Okwi akiteswa na hat trick hiyo, naye Alex Kitenge wa Stand United, ameingia kwenye mkumbo huo baada ya kufunga hat trick uwanjani hapo dhidi ya Yanga.
Kitenge alifanya hivyo Septemba 16, 2018, wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 4-3. Tangu wakati huo, mpaka leo Kitenge hajafunga bao lolote akiwa na mabao matatu.
The post Hat Trick Yamtesa Okwi Simba SC appeared first on Global Publishers.