Najua Ngoma kama Goroka, Mikogo Sio, Namwaga Mboga, sio nyimbo ngeni masikioni mwako kwani ni nyimbo zilizotokea kupendwa sana na kuwa Hits Song kwa muda mrefu, lakini swali ni je unamjua aliyeimba nyimbo hizo?
Asilimia kubwa ya mashabiki wake hawamfahamu kwa sura na pengine hata jina lakini wanapenda sana ngoma zake, Anaitwa Jay Melody, mkali kutoka THT, ambaye pia mbali na kuimba ni mwandishi mzuri na ameshaandika nyimbo za wasanii wakubwa kama vile Kivuruge ya Nandy, Hauzimi ya Benson na nyingine nyingi.
Usiku wa Desemba 31, katika uwanja wa Taifa wa Burudani alipata fusra ya kupafomu kwenye tamasha la Tunafunga Jumla Jumla lililoandaliwa spesho kwa ajili ya Rostam na Maua Sama.
katika tamasha hilo Jay Melody akapiga stori na Global TV na kueleza kwanini nyimbo zake zinamzidi ukubwa.
The post “NANDY Nishafanya Nae / Hawajui / ROSTAM tumetoka Mbali” – JAY MELODY – VIDEO appeared first on Global Publishers.