NEWS

1 Juni 2019

Picha Mkewe Pasta Ng'ang'a Ambaye Amezua Utata Baina yake na Wachungaji wa Kanisa Lake

Mtumishi mwenye utata Maina Ng'ang'a kwa mara nyingine tena amegonga vichwa vya habari baada ya kuwapa msomo baadhi ya wafuasi wake kwa madai ya kummezea mate na kumkosea heshima mkewe. Kufuatia matamshi yake, pasta huyo ameshambuliwa vikali na baadhi ya wakenya ambao wanahisi kwamba kazi yake katika dini inaelekea kutumbukia. 

Lakini, ni mke yupi huyu ambaye amemfanya Ng'ang'a kupandwa na mori kiasi cha kuwatusi na kuwatishia waumini na maaskofu kanisani mwake? 

 Ng'ang'a amemuoa Loise Murugi Maina ambaye anahudumu katika mojawapo ya matawi ya kanisa lake.