NEWS

1 Juni 2019

Siwema wa Nay wa Mitego Akanusha Kumtelekeza Mwanaye


MZAZI mwezie na mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay’, Siwema Edson amekanusha madai ya kutomtembelea mwanaye Cartes.


Akizungumza na gazeti hili, Siwema alisema huwa ana ratiba maalum ya kwenda kumuona mwanaye huyo ambaye anaishi na bibi yake, ambaye ni mama yake na Nay, ila anapokwenda huwa hamjulishi mzazi mwenzake huyo.


“Mtoto wangu naongea naye kila mara na nimeshaenda kumuona zaidi ya mara tatu, sema tu baba yake hajui hivyo angekuwa anamuuliza mama yake angempa jibu, lakini mwanangu nishamuona na ninaongea nae kila mara,” alisema Siwema.

Stori: Imelda Mtema