Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kufuatia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililotelewa na Waziri mkuu wa jamhuri ya muungnao wa Tanzania Mh Kasim Majaliwa wananchi jijini Dodoma wamejitokeza kusalimisha mifuko ya plastiki katika kampuni ya usafi ya Green waste tawi la Dodoma ambayo imefanya uzinduzi wa vituo vya kukusanya mifuko ya plastiki.
Akizungumza katika uzinduzi wa vituo vya kupokea mifuko ya plastiki mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bwana Godwin Kunambi amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutii sheria kwani wameunda kamati mbalimbali ambayo itapita kila nyumba na maduka ili mifuko ya plastiki .
Aidha kunambi ameongeza kuwa Jiji la Dodoma limetoa elimu ya mifuko ya plastiki katika ngazi ya Mtaa,Kata,Wilaya na Taasisi zote za jiji huku akisema zipo baadhi ya taasisi zinashindwa kulipa hela ya usafi
Akizundua vituo vya kupokea mifuko ya plastiki Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Bwana Patrobas Katambi Ambaye ndiye mgeni rasmi katika uzinduzi huo amesema kuwa wajibu wa kutunza mazingira ni jukumu la kila mwananchi ambpo amesema kuwa kwa taasisi ambazo hazilipi tozo za taka watachukuliwa sheria.
Kwa upande wake Ally Mfinanga ambaye ni Afisa Mazingira wa Jiji la Dodoma amesema kuwa kwa atakaye bainika kuzalisha na kuingiza mifuko faini yake itakuwa ni shilingi milioni 20.
Hatahivyo, Katambi amesema kuwa jiji la Dodoma halitakuwa na msamaha kwa mtu yeyote atakaye kutwa na mfuko wa plastiki huku akisema kuwa watu ambao wanauza mifuko hiyo waisalimishe katika vituo ambavyo vinapokea mifuko hiyo.
Ikumbukwe kuwa Mwisho wa Matumizi ya Plastiki hapa nchini ilikuwa jana Mei.31 2019 na atakayebainika anauza au kutumia mfuko wa Plastiki kuanzia leo Juni 1,2019 hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.