NEWS

31 Julai 2019

Barnaba avinjari na mpenzi mpya, "hajui Kiswahili"


Bosi wa lebo ya muziki ya High Table Sound, Barnaba Classic, ameonekana akijiachia na mpenzi wake mpya kwenye moja ya klabu za starehe Jijini Dar es Salaam.


Barnaba ameonekana baada ya kunaswa na kamera za EATV akiwa na mpenzi wake huyo katika usiku wa show ya Lulu Diva, na kusema kuwa mpenzi wake huyo hajui kuongea Kiswahili.

“Hajui Kiswahili, hawezi kuongea ana matatizo ya koromeo, ahsante sana”, amesema Barnaba.

Mpenzi huyo wa Barnaba hajafahamika jina lake na wala hajulikani kama anatokea nchi gani mpaka sasa.

Kabla ya mpenzi wake huyo mpya, Barnaba Classic aliwahi kuwa katika ndoa na Mke wake Mama Steve na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Steve na waliachana miaka kadhaa iliyopita.