NEWS

31 Julai 2019

AY, Mwana FA waelezea ugumu wa ndoa za mastaa


Wasanii wakubwa na marafiki wa muda mrefu kutokea hapa nchini Tanzania AY na Mwana FA, wametoa somo kwa watu wote kuhusu maisha ya urafiki wao pamoja na maisha ya ndoa zao.

Wakiongea hayo kupitia Super Mix ya East Africa Radio, AY na Mwana FA waliulizwa kuhusu ugumu wa mastaa kuishi katika ndoa, urafiki wao na maisha kiujumla, ambapo Mwana FA amesema,

“Kuna ugumu wa ustaa na maisha ya ndoa, ugumu upo hasa unapotaka kujichanganya na watu, kuna wakati mwingine huwezi kuongea na simu usiku, sababu ya mke wangu kwa sababu huwa najua niko kwenye upande wa familia”.

Baada ya kusema hivyo, AY naye akazungumzia kuhusu urafiki wao akisema urafiki ni lazima watu wafahamiane na wakubaliane, kutokuwa wabinafsi, kumfikiria mwenzako kwenye upande wa maendeleo. Pia akaendelea kusema yeye na Mwana FA walianza urafiki wao tangu mwaka 2002, pia urafiki wao umechangia kuleta mafanikio na maendeleo.

Aidha kuhusu maisha yao binafsi, wawili hao huwa wanatofautiana lakini kila mmoja anasimamia misimamo yake, ndiyo maana kila mtu anaficha kasoro za mwenzake, pia ni ni kutokana na historia ya maisha yao inayofanana.