NEWS

31 Julai 2019

Global FC kukipiga na Kili Veterani Ijumaa

TIMU tajiri yenye mastaa kibao wanaowindwa na timu za daraja la kwanza na la pili, Global FC imehamishia hasira kwa Kilimanjaro Veteran. Global FC iliyoko chini ya Kocha Amran Kaima ‘Zahera’ katika mchezo uliopita walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na timu ya Sinza Boys inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu mkoa.

 

Kwa mujibu wa habari za ndani ya uongozi wa Global FC, Zahera analazimika kushinda mchezo huo ili kulinda kibarua chake baada ya wadau kuanza kuhoji mbinu zake haswa kutokana na ubora wa timu aliyonayo. Mdhamini wa timu ya Global FC, kampuni ya Ashishi Cinematographer, ameiahidi zawadi mbalimbali kwenye mchezo huo.

 

Mdhamini huyo amekuwa akivutwa na uchezaji mzuri wa Global FC, jambo ambalo limemfanya kupagawa na kuahidi kutoa mengi zaidi ya hayo.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Saleh Amir alisema kuwa atatoa vitu vingi kwa timu hiyo kutokana na kufurahishwa na kiwango cha uchezaji haswa kwa jinsi inavyotoa dozi kwa wapinzani wake ambao wanacheza nao.

MAMA DIAMOND – “DIAMOND MADAWA ya Kulevya ANGEANZIA Tandale”

The post Global FC kukipiga na Kili Veterani Ijumaa appeared first on Global Publishers.