Huko nchini Ngeria, watu 65 wameuawa baada ya Kikundi cha Kigaidi cha wanamgambo wa Boko Haram kufanya shambulio katika shughuli ya mazishi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kiongozi wa Serikali katika eneo la Borno ya Kaskazini, Muhammed Bulama amesema kuwa watu 10 wamejeruhiwa na wanaendelea kupatiwa matibabu
Shambulio hili limetajwa ni la kulipa kisasi baada ya Wanakijiji kuwaua wapiganaji 11 wa Boko Haram na kuwanyang’anya silaha zao.
”Ni watu 65 wamefariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa vibaya, amesema Muhammed Bulama Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji kilichovamiwa.
Ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotokewa ni kwamba watu 23 waliuawa wakati wakitoka kwenye mazishi na wengine 42 waliuawa wakati wa mapambano na magaidi hao.
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari jumapili aliamua kutoa majashi yake na kuyatuma kufanya msako wa kuwakamata magaidi hao.
Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa magaidi wa Boko Haram kuvamia na kufanya mauaji katika wilaya ya Nganzai.
Ndani ya muongo 1 mashambulio ya Boko Haram yameua watu 27,000 na kusababisha zaidi ya watu milioni 2 wayakimbie makazi zao