Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amekiri kuwa sauti iliyovuja mitandaoni wiki mbili zilizopita ni ya kwake.
Membe amesema sauti hiyo ni ya kwake kwa asilimia 100 na maongezi ni yake binafsi, Hivyo amesema anajua ni wapi kulipotokea tatizo.
Membe amesema kuwa udukuaji ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria zetu hapa Tanzania. Kutokana na hilo ameamua kuwaachia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wafanye kazi hiyo.