Mahakama ya Kisutu imekataa na imeutaka upande wa Serikali kuwasilisha kiapo kinzani kabla ya August 5, 2019 kujibu hoja kuhusu kukamatwa kwa Mwanahabari Erick Kabendera.
Wakili wake Shilinde Swedy amewasilisha maombi ya kutaka Kabendera afikishwe Mahakamani kwasababu anashikiliwa kwa zaidi ya masaa 24 tangu July 29.
Upande wa Jamhuri ulitaka kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani Agosti 7, mwaka huu, lakni Mahakama ikakataa.

Jamhuri wamekutana na kikwazo hicho leo Alhamisi saa tatu asubuhi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile anayesikiliza maombi hayo.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai maombi hayo yaliwafikia jana na leo shauri linakuja kwa mara ya kwanza hivyo anaomba apewe muda wa kuwasilisha kiapo cha majibu kinzani Agosti 7 mwaka huu kwa sababu kesho atakuwa Mahakama Kuu katika kesi nyingine.
Wakili wa mwombaji, Shilinde Swedy alidai mteja wake yuko chini ya ulinzi kwa zaidi ya saa 24, hajapata uwakilishi wa aina yoyote hivyo aliomba kesi ije Jumatatu.
Hakimu Rwizile alisema kwa kuwa maombi yamekuja chini ya hati ya dharura, muda ulioombwa na Jamhuri ni mrefu, hivyo maombi hayo yatasikilizwa Agosti 5, mwaka huu.
“Maombi yatasikilizwa Agosti 5, mwaka huu siku ya Jumatatu saa saba mchana, wajibu maombi watajibu wakati wowote kabla ya muda huo,” amesema Hakimu Rwizile.