NEWS

29 Desemba 2019

Chanzo Cha KIFO cha Faru Fausta Chaelezwa


Imebainika kuwa Faru Fausta alifikwa na mauti, baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi vizuri.

Hiyo ni kwa kwa mujibu wa taarifa ya upasuaji uliofanywa na jopo la madaktari wa wanyamapori na wataalamu wengine wa uhifadhi kutoka taasisi ya utafiti wa Wanyamapori nchini na hifadhi ya Ngorongoro.

Daktari wa Wanyamapori, Robert Fyumanga amesema kuwa kuta za moyo wa Faru Fausta, zilikuwa nyembamba sana hali iliyopelekea damu ishindwe kupita kwa ufasaha.

"Kuta za Moyo wake zimekuwa ni nyembamba sana hivyo kushindwa kusukuma damu ya kutosha mwilini, kwahiyo alikosa nguvu na kuanguka" amesema Dkt Fyumanga.

Ikumbukwe Faru jike mweusi ambaye alipewa jina la Fausta, ambaye pia alikuwa akitajwa kama Faru mzee kuliko wote duniani, alikufa hapo jana Disemba 28, 2019 katika eneo alilokuwa akihifadhiwa.