NEWS

29 Aprili 2020

Lema Awalipua Wanaomzushia Kupata Corona



Baada ya taarifa kusamba kwenye mitandao ya kijamii kuwa mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema amepata maambukizi ya ugonjwa wa Corona mbunge huyo amewataka wanaosambaza taarifa hizo kupiga kelele za kuokoa maisha ya watanzania na si vinginevyo

Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Lema amesema hawezi kutolewa kwenye mjadala wa Corona kwa sababu ya taarifa za uzushi

“MATAGA mnafikiri mnaweza kututoa kwenye mjadala wa CORONA VIRUS kwa ujinga wenu.Watu wana kufa,pigeni kelele kuokoa maisha ya watu ili walioko vijijini warudi mjini.Tutapiga kelele usiku/ mchana,bila kumuogopa mtu.Niko sawa na nitaendelea kuwa sawa kwani Mungu analo  kusudi nami” ameandika